Makala

Ifahamu filamu ya Armageddon (1998)

0
filamu ya Armageddon
filamu ya Armageddon

Moja ya sinema ambayo mpaka leo napenda kuiheshimu kutokana na jinsi Wamarekani wanavyotengeneza uzalendo kwa watu kuhusiana na suala la ujasiri wa mwanadamu katika mambo magumu kabisa ukiachia sinema ya Independence na Air Force One ni hii sinema ya Armageddon , sinema ambayo imetoka 1998.

Sinema hii iliyonakshiwa (kutengenezwa) na Michael Bay inatembea kwa dakika 144. Humu ndani unakutana na Bruce Willis, Billy Bob Thornton, Liv Tyler, Ben Affleck na wengineo wengi katika sinema ambayo inazungumzia maangamizi ya dunia yatakayosababishwa na magimba maarufu katika lugha ya kawaida kama vimondo.

Kuna sinema nyingi zimetengenezwa katika kile ambacho mimi nakiita hofu ya mwanadamu ya kuangamizwa na majabali ya anga za juu.

Lakini sinema zote hizo ikiwamo ya mwaka 1979 Meteor ambapo mkali Sean Connery alikuwa kinara Deep Impact ya akina Morgan Freeman na mwenzake Robert Duval ya mwaka 1998, haziwezi kuivuruga hii ambayo imejaa pia mambo yanayohusu mapenzi na familia.

Kwenye picha hii Bruce Willis akicheza kama Harry S. Stamper ,Billy Bob Thornton kama Dan Truman,Ben Affleck kama A.J. Frost ,Liv Tyler kama Grace Stamper na Will Patton kama “Chick’’ Chapple wameitendea haki sinema hii iliyuoandikwa na Jonathan Hensleigh akishirikiana na J.J. Abrams.

Soma pia:  Pierre Liquid kula shavu Marekani

Picha hii imeigizwa wakati hofu tayari ilishatanda katika dunia ya kwamba mwisho wa dunia ni Desemba 31,1999 . Baadhi ya makundi ya dini na wataalamu wa masuala ya ufundi( usiulize) walitabiri kwamba dunia inamalizika na kitu kingine kinazaliwa.

Hii si mara ya kwanza kuwepo na hofu hiyo kwani wakati wa karne za kati kulizuka pia hofu wakati dunia ilipokuwa inasubiri kurejea mara ya pili wa Kristo kama ilivyobashiriwa katika Biblia.

Lakini pamoja na yote hayo kuna maneno ambayo yanazungumzwa kuhusu ujio wa mpinga Kristo huku vita kali ikiwa angani kati yake na malaika, hii inaitwa Armageddon.

Hofu ya kumalizika kwa dunia haipo huko tu lakini majanga ya asili na pia silaha z aatomiki zinaiweka dunia katika mtego wa kujiangamiza yenyewe kwa milipuko, Dk Strangelove kwenye “Doomsday Machine” akicheza kama Vera Lynn au tuseme Terminator 2 kwenye Judgment Day wanaonesha namna ambavyo itakuwa ngumu kupona katika vita vya nyukilia.

Soma pia:  Sera za Uhamiaji za Trump kumgusa 21 savage

Kuna mambo mengi yametengenezwa sinema kueleza hofu ya mwandamu katika ardhi na mazingira yake na sinema chache zimezungumzia tishio kutoka anga la juu na ndio unaona vitu kama War of the Worlds, Independence Day na hii ambayo nimeipenda ya Armageddon.

Masuala mengi yanaleta hofu duniani na kusema imekuwaje mijusi mikubwa imetoweka duniani kwan ini sisi tusitoweke kwa mtindo huo huo? Ndani ya Armageddon jabali lenye ukubwa wa jimbo la Texas linaelekea kuitandika dunia.

Mtaalamu mmoja anasema jabali lile na ukubwa wake ndilo lililoangamiza ile mijusi mikubwa.

Mkurugenzi wa NASA nafasi iliyochezwa na Billy Bob Thornton anasema wananchi wa Marekani wasiwe na hofu kwani wana watu kama Bruce Willis wanaoweza kujitolea na teknolojia ya kutosha kukabili hali hiyo kutoka NASA.

Jambo ambalo ni lazima ukumbuke ni kwamba katika suala la kuhami dunia teknolojia ambayo inatarajiwa kuiangamiza dunia ndio inayotumika kutaka kukoa, nguvu za nyukilia. Jabali lazima lipasuliwe na nguvu za atomiki.

Soma pia:  Rihanna Awaza kuwa Mwanamitindo

Nusu ya pili ya sinema kama utazigawa, zinakutambulisha teknolojia na mambo yanayoambatana nazo kukupa ile freshi ambayo unahitaji kuijua wakikufanya uamini nini kinatokea huku maisha sehemu nyignine yakiendelea.

Pamoja na Wamarekani kujimwambafai ( kujikuza mno) katika hili kuna ukweli kuwa ukuaji wa sayansi za anga za juu Marekani huenda ikawa suluhu ya mambo mengine yanayotishia dunia kutoka anga za juu.

Kama wewe si mtu wa kupenda vifereji vya sauti vyenye kiki kubwa, unaweza kuwa na shida lakini ninachotaka kusema ni kwamba nimeipenda sinema hii yenye kuangalia hatima ya binadamu katika maisha yake na uzuri.

Ni moja ya sinema zilizolisha vyema dunia kuhusu shaka pamoja na kwamba kuna vitu vingi vinakwenda ndivyo sivyo kwa wale wanaopenda kuangalia sienma za sayansi ataona vipimo vya sienma hii vimejaa na kusukasuka hasa baba mkwe anapoona vyema kutekeleza ahadi ya mtoto wake, kumrejesha salama mchumba wake.

Comments

Comments are closed.

More in Makala