Michezo

Drogba: Lukaku atafanya maajabu Kombe la Dunia 2018

0
Lukaku atafanya maajabu Kombe la Dunia 2018
Romelu Lukaku

Mshambualiaji wa zamani wa timu ya Chelsea, Didier Drogba, amesema ana imani nyota wa Ubelgiji, Romelu Lukaku, atafanya maajabu makubwa katika Kombe la Dunia linaloendelea nchini Russia.

Drogba, amesisitiza kuwa Lukaku atakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na kiwango alichokionyesha kwenye mechi mbili za kwanza katika kundi G.

Nyota huyo anayeichezea Manchester United, amefunga mabao manne kwenye mechi mbili za hatua ya makundi ambapo ameingia kwenye orodha ya kuwania kiatu cha dhahabu na wenzake Cristiano Ronaldo wa Ureno na Straika wa Uingereza, Harry Kane ambao wote wana mabao manne kila mmoja.

Drogba alisema alizungumza na Lukaku na kumhakikishia kuwa atafanya maajabu kwenye michuano ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuibuka mfungaji bora.

Soma pia:  Guardiola amtetea Sarri na kipigo

Alisema Lukaku ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ana mwili mzuri wa kukabiliana na mabeki kila wakati.

“Lukaku atafanya maajabu makubwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuibuka mfungaji bora, kuna upinzani kati yake, Kane na Ronaldo lakini ninakiamini kiwango chake,” alisema Drogba.

England kesho itavaana na Ubelgiji kwenye mchezo wa mwisho katika kundi G. mechi hiyo itaamua timu gani imalize kileleni mwa msimamo wa kundi hilo.

Romelu Lukaku Kombe la Dunia
Romelu Lukaku akiwa na Ubelgiji kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018

Comments

Comments are closed.

More in Michezo